spacer
International_25_no text
spacer

A selection of testimonials from our satisfied customers.
Satisfied Customers

keyline

Swahili

Hague ni mtoa huduma anayeongoza duniani wa chapa za usalama, na suluhisho za kiusalama. Hague, iliyoanzishwa mwaka 1980 na inayomilikiwa kibinafsi, ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Viwanda binafsi vinavyotoa chapa (IPIA) na pia ni mwanachama kamili wa Umoja wa watengenezaji wa Hologramu wa kimataifa (IHMA) na taratibu zetu za uongozi zinazingatia kikamilifu BS EN ISO 9001:2008.

Hague hutoa suluhisho za kipekee na zisisho mwisho kwa ajili ya wateja katika nchi zaidi ya 30 kwa kuweka kituo kimoja cha mawasiliano kwa ajili ya kutoa suluhisho za chapa salama zenye viwango vya hali ya juu, bunifu na za kibinafsi. Orodha ya wateja wetu ni pamoja na mabenki, serikali, vyuo vikuu, na wateja wenye majina makubwa na maarufu duniani.

Jalada la Hague la Usalama linayo pamoja na:-

Chapa ya Usalama – inasambaza mamilioni ya nyaraka za usalama, mamilioni ya vyeti/hati salama za vyuo vikuu, pia inasambaza makumi kwa mamilioni ya hundi zilizoidhinishwa na APACS na mamia kwa mamilioni ya stakabadhi salama za hazina (Stempu za Ushuru).

Jaribosi salama za hologramu - na hologramu salama za muundo wa pekee zilizosajiriwa, kadi za vitambulisho, vyeti/hati, kadi za ATM, Misokoto Salama ya joto ya ETR (Premierreceipts) misokoto iliyobinafsishwa ya ATM, nyaraka za biashara, ulinzi wa nembo na suluhisho salama za nyaraka.

Programu ya Usalama – pamoja na hundi za nembo za Premier PREMIERcheque+, na vijitabu vyake PREMIERchequebook+, programu zilizoundwa kwa ajili ya Printa za TROY MICR zilizoidhinishwa na APACS kwa ajili ya kutoa na kujaza cheki za usalama wa hali za juu, vitabu vya hundi na nyaraka za usalama. PREMIERcert+ hutoa taratibu za kuthibitisha uhakika wai vyeti vya Vyuo vikuu kupitia wavuti.

Vifaa vya Usalama – Vifaa maalumu vya usalama vyenye viwango vya hali ya juu vya kuzuia na kudhibiti dhidi ya udanganyifu pamoja na kifaa maalum cha mezani cha Hague cha kuweka hologramu kinachoitwa Securogram© pamoja na vifaa vinginevyo vya usalama wa nyaraka kama vile vilinda viwango, vipenyeshaji na vitia saini hundi. Skana za taswira/picha na vifaa vinavyosoma mistari ya msimbo pia vinasaidia kuboresha uchakataji na upatanishaji wa nyaraka.

Hague inatoa ushauri, programu changamani, suluhisho za viwango vya hali ya juu pamoja na vifaa vya kuzuia udanganyifu. Hague inaweka kituo kimoja cha kuaminika cha mawasiiano kwa ajili ya kuhifadhi data na nyaraka zako muhimu popote duniani, tunatoa huduma zinazokidhi mahitaji yako na ambazo zitahakikisha bidhaa, huduma, biashara, wafanyikazi na wateja vyote vinakuwa salama.